1 Corinthians 4:18-21

18 aBaadhi yenu mmekuwa na jeuri mkidhani kuwa sitafika kwenu. 19 bLakini kama Bwana akipenda, nitafika kwenu mapema, nami nitapenda kujua, si tu kile wanachosema hawa watu jeuri, bali pia kujua nguvu yao. 20 cKwa kuwa Ufalme wa Mungu si maneno matupu tu bali ni nguvu. 21 dNinyi amueni. Je, nije kwenu na fimbo, au nije kwa upendo na kwa roho ya upole?
Copyright information for SwhKC